Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wizara ya Katiba na Sheria

Mhe. Chana Awasilisha Taarifa ya Utekelezaji ya Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora.

Imewekwa: 08 Nov, 2023
Mhe. Chana Awasilisha Taarifa ya Utekelezaji ya Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora.

Na George Mwakyembe - WKS Dodoma.

Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Balozi Dkt Pindi Chana amewasilisha taarifa ya utekelezaji wa majukumu ya Tume za Haki za Binadamu na Utawala bora kwenye Kamati ya Kudumu ya bunge ya Utawala, Katiba na Sheria. Katika taarifa hiyo Mhe. Chana amefafanua kuwa utekelezaji wa majukumu ya Tume ni ya mtambuka kwani yanagusa maisha ya binadamu ya kila siku.

Mhe. Chana amewasilisha taarifa hiyo tarehe 07 Novemba, 2023 katika ukumbi wa Bunge Jijini Dodoma. Akifafanunua kwenye kikao Mhe. Chana amebainisha kuwa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora ni taasisi ambayo ni ya Muungano na imekuwa ikishughulikia masaula yote ya haki za binadamu Tanzania Bara na Tanzania Zanzibar.

Naye Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora Jaji Mstaafu Mathew Mwaimu amewambia wajumbe wa Kamati hiyo kuwa Tume imekuwa ikisimamia masuala ya haki za binadamu pamoja na utawala bora lakini changamoto wanayopata ni upungufu wa watumishi. Pia Tume imekuwa ikipata changamoto ya kutokupata taarifa pindi matukio ya ukiukwaji wa haki za binadamu yanapotokea.

Akichangia kwenye uwasilishwaji Makamu Mwenyekiti wa Tume Mohamed Hamad amewashukuru wajumbe kwa kuwapa ushirikiano lakini pia kuwaongezea bajeti ukilinganisha na miaka ya nyuma na tayari wamefungua ofisi nyingine Zanzibar ili kuhakikisha tunashughulikia msauala ya haki kwa pamoja.