Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wizara ya Katiba na Sheria

Mswada Sheria ya Ndoa Kuingia Bungeni

Imewekwa: 05 Apr, 2023
Mswada Sheria ya Ndoa Kuingia Bungeni

Farida Khalfan & Lusajo Mwakabuku - WKS

Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro amekutana na kufanya mazungumzo na Jukwaa la Wakurugenzi Wanawake waliowakilisha mashirika takribani 400 yanayotetea haki za wanawake, wasichana na watoto nchini Tanzania, tarehe 05 Aprili, 2023 ofisini kwake, Mtumba Jijini Dodoma.

Kupitia kikao hicho Waziri ameeleza nia ya Serikali kupitia Wizara ya Katiba na Sheria kupeleka muswada wa mabadiliko ya Sheria ya Ndoa, 1971 katika Bunge hili la bajeti, ili kuweka umri wa miaka 18 kama umri wa chini wa kuolewa na kuoa kama ilivyoelekezwa na Mahakama.

Aidha, Wakurugenzi kutoka Jukwaa la Wakurugenzi Wanawake walitumia fursa hiyo kumhakikishia Waziri na ofisi yake ushirikiano katika kuhakikisha mchakato huo unapelekea kuwa na Sheria nzuri yenye mlengo wa kijinsia kwa ajili ya kuimarisha ulinzi kwa watoto hasa watoto wa kike.