Pindi Chana Afungua Mafunzo ya Makatibu Tawala wa Wilaya

Na Mwandishi Wetu - Njombe
Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chana leo Juni 27, 2024 amefungua mafunzo kwa Makatibu Tawala wa Wilaya kuhusu shughuli za Usajili wa Vizazi, Vifo, Ndoa, Talaka na Udhamini yaliofanyika katika ukumbi wa Agreement mkoani Njombe.
Mhe. Pindi Chana akifungua mafunzo hayo amesisitiza juu ya umuhimu wa Usajili wa matukio muhimu ya binadamu kama vizazi, vifo na sababu zake, ndoa na talaka kwani takwimu hizo zinasaidia Serikali katika kupanga maendeleo.
“Tumekuwa tukizitumia takwimu hizi katika kupanga mipango mbalimbali ya maendeleo na huduma kwa jamii, hivyo natoa maelekezo kwa Ofisi zote za Mikoa ndani ya Tanzania Bara ziwe zinaandaa taarifa za robo mwaka za usajili wa matukio muhimu ya Binadamu ambazo zitabainisha Mafanikio na changamoto na kuziwasilisha RITA ili ziweze kufanyiwa kazi.” Alisema.