Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wizara ya Katiba na Sheria

Prof. Kabudi Afanya Kikao na Balozi wa Urusi Nchini

Imewekwa: 27 Sep, 2024
Prof. Kabudi Afanya Kikao na Balozi wa Urusi Nchini

Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Prof. Palamagamba John Kabudi leo 27 Septemba, 2024 jijini Dar es Salaam amekutana na kufanya kikao na Balozi wa Urusi Nchini Bw. Andrey Avetisyan kujadili maeneo mbalimbali ya kiuchumi na kidiplomasia kwa lengo la kuleta maendeleo kwa jamii.

Akizungumza katika kikao hicho Mhe. Kabudi amesema kuwa mbali na urafiki na ushirikiano uliopo baina ya Nchi hizi mbili wanaendelea kuangalia maeneo muhimu ya kuboresha ikiwemo ushirikiano kwenye masuala mbalimbali ikiwemo la utoaji wa huduma za haki ambalo liko chini ya mamlaka ya Wizara ya Mambo ya Katiba na Sheria, elimu, utamaduni, ulinzi, utalii, afya, biashara na uwekezaji.

Aidha Bw. Avetisyan amesema kuwa Urusi itaendelea kushirikiana na Tanzania ili kuimarisha zaidi mahusiano yaliyopo ili kuboresha upatikanaji wa haki na kupambana na uhalifu kwa njia ya mtandao.