Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wizara ya Katiba na Sheria

Rais Samia Achangia Ujenzi wa Kanisa la Mt. Barnaba - Ngumbo.

Imewekwa: 20 Aug, 2023
Rais Samia Achangia Ujenzi wa Kanisa la Mt. Barnaba - Ngumbo.

Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro ameshiriki katika Ibada ya Harambee ya Ujenzi wa Kanisa la Anglikana la Mtakatifu Barnaba - Ngumbo lililopo Kijiji cha Ngumbo, Wilaya ya Nyasa.

Katiba Ibada hiyo iliyofanyika tarehe 20 Agosti, 2023 na kuhudhuriwa pia na Mhe. Filberto Sanga, Mkuu wa Wilaya ya Nyasa, Mhe. Ndumbaro amewaasa wananchi wa Kijiji cha Ngumbo kuendelea kumcha Mungu na kumjengea Mungu nyumba ya Ibada kwa kuwa Mungu mwenyewe katika Maandiko Matakatifu ameahidi kutuletea amani kupitia nyumba za Ibada huku akiwaasa viongozi kutekeleza majukumu yao ya kiroho na si kutumika kisiasa kunakopelekea kuwachanganya waumini wanaowaongoza.

Katika Ibada hiyo Mhe. Ndumbaro amewasilisha salaam za Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye ameunga mkono juhudi za ujenzi wa Kanisa hilo kwa kuchangia Shilingi Milioni Tano.