Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wizara ya Katiba na Sheria

TAWLA yafanya Mkutano Mkuu wa 33

Imewekwa: 08 May, 2023
TAWLA yafanya Mkutano Mkuu wa 33

Mhe. Pauline Gekul Naibu Waziri wa Katiba na Sheria ameshiriki ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa 33 wa Chama cha Wanasheria Wanawake Tanzania (Tanzania Women Lawyers – TAWLA) uliofanyika tarehe 06 Mei, 2023 Jijini Dar es Salaam. Mgeni Rasmi katika mkutano huo alikuwa Mhe. Dkt. Tulia Ackson, Spika wa Bunge la Tanzania. 

Katika hotuba yake Naibu Waziri, alisisitiza kuwa Serikali kupitia Wizara ya Katiba na Sheria itaendelea kushirikiana na TAWLA hususan katika kupokea mapendekezo na maoni ya marekebisho mbalimbali ya sheria.