Tume ya Kurekebisha Sheria Yakabidhi Ripoti za Tafiti Katika Sekta ya Sheria
Tume ya Kurekebisha Sheria Yakabidhi Ripoti za Tafiti Katika Sekta ya Sheria
Imewekwa: 26 Mar, 2025

Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro tarehe 24 Machi, 2025 amepokea taarifa mbili za tafiti za Sheria mbalimbali kutoka kwa Mwenyekiti wa Tume ya Kurekebisha Sheria Tanzania Mhe, Jaji Winfrida Korosso
Taarifa hiyo imehusisha mapitio na utafiti wa Sheria mbalimbali kwa mwaka 2023/2024 na mwaka 2024/2025 ikihusisha taarifa ya mapitio ya Takwimu Sura 351 na ya pili ikiwa ni taarifa ya Utafiti kuhusu Mfumo wa Sheria zinazosimamia Vyama vya Ushirika.