Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wizara ya Katiba na Sheria

Tume ya TEC Yakutana na Kabudi na Katambi

Imewekwa: 07 Nov, 2024
Tume ya TEC Yakutana na Kabudi na Katambi

Jopo la wawakilishi wa Tume ya Kimisionari ya Baraza la Maaskofu wa Kanisa Katoliki (TEC) limekutana na Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Prof. Palamagamba John Kabudi na Mhe. Patrobas Katambi, Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu - Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu kuzungumzia juu ya taarifa ya takwa la marekebisho ya sheria kuhusu wamisionari wa kikatoliki Tanzania wenye uraia wa nje.

Mazungumzo hayo yanafuatia ombi lililotolewa na Askofu Mkuu wa Songea na Mwenyekiti wa Tume ya Kimisionari ya Baraza la Maaskofu wa Kanisa Katoliki (TEC) Askofu Damian Dallu kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan alipofanya ziara ya kikazi na kufanya mazungumzo na viongozi wa dini mjini Songea mwishoni mwa mwezi Septemba mwaka huu Mkoani Ruvuma.

Mazungumzo hayo yamefanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Wizara ya Katiba na Sheria Mtumba leo tarehe 07/11/2024 na kushuhudiwa na Katibu Mkuu Bwana Eliakim Maswi na baadhi ya wajumbe wa Menejimenti ya Wizara.