Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wizara ya Katiba na Sheria

Tumejipanga - Mtaka & Chana

Imewekwa: 22 May, 2024
Tumejipanga - Mtaka & Chana

Na Lusajo Mwakabuku – WKS Njombe

Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chana na Mkuu wa Mkoa wa Njombe Mhe. Anthony Mtaka kwa pamoja wamesema wamejiandaa kikamilifu katika kuhakikisha kuwa wananchi wa Tanzania wananufaika na Kampeni ya Msaada wa Kisheria maarufu kama "Mama Samia Legal Aid Campaign"

Viongozi hao wameyasema hayo Mei 22, 2024 walipokuwa wakizungumza na Waandishi wa habari katika  ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Njombe juu ya uzinduzi wa kampeni hiyo mkoani humo.

Utekelezaji wa Kampeni hiyo ulianzia jijini  Dodoma ambapo ilizinduliwa tarehe 27 Aprili, 2023, na Zanzibar tarehe 9 Mei, 2023.

Kwa sasa Kampeni hii imeufikia Mkoa wa Njombe ambapo huduma za msaada wa kisheria zitatolewa bure kwa Wananchi katika Halmashauri zote sita kuanzia tarehe 26 Mei, 2024.