Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wizara ya Katiba na Sheria

Tunaandaa Mkutano wa Viwango vya Juu - Dkt. Chana

Imewekwa: 06 Feb, 2024
Tunaandaa Mkutano wa Viwango vya Juu - Dkt. Chana

Na William Mabusi – WKS Dodoma

Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chana, amepitishwa kwenye taarifa ya maandalizi ya Mkutano wa Mawaziri wa Sheria kutoka nchi za Jumuiya ya Madola, tarehe 05 Februari, 2024 Dodoma na kuahidi kuandaa mkutano utakaokuwa wa viwango vya juu kwani tayari uwezo wa kuandaa mikutano ya kimataifa Wizara unao ambapo mwishoni mwa mwaka 2023 Wizara iliratibu kikao cha 77 cha Kamisheni ya Haki za Binafamu kilichofanyika mkoani Arusha kwa siku 21.

“Tutafanya Maandalizi mazuri na kwa Viwango vya Kimataifa kwa heshima ya Nchi yetu.” Alisema Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chana, Waziri wa Katiba na Sheria akilezea mkutano huo utakaofanyika kuanzia tarehe 04 – 08 Machi, 2024 Zanzibar.