Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wizara ya Katiba na Sheria

UFUATILIAJI NA TATHMINI UIMARISHE UWAJIBIKAJI NA UWAZI

Imewekwa: 25 Sep, 2025
UFUATILIAJI NA TATHMINI UIMARISHE UWAJIBIKAJI NA UWAZI

Katibu Mkuu Wizara ya Katiba na Sheria Eliakim Maswi amewataka watumishi wa Wizara hiyo kutumia ufuatiliaji na tathmini kama nyenzo ya kuimarisha ufuatiliaji, uwajibikaji na matumizi bora ya rasilimali.

Maswi ameyasema hayo Septemba 24, 2025 baada ya mafunzo ya umuhimu wa kufanya ufuatiliaji na tathmini yaliyofanyika katika ukumbi wa Wizara hiyo Mtumba jijini Dodoma ambapo ameongeza kuwa mafunzo yawezeshe watumishi kujipima utendaji wao.

Ameongeza kuwa baada ya mafunzo hayo anatarajia kuona matokeo Chanya yenye manufaa kwa wananchi kwakuwa ufuatiliaji na tathmini ni moyo wa taasisi unaowezesha kuimarisha uwajibikaji ili Wizara iweze kutimiza majukumu yake ya msingi.

Kwa upande wao watumishi wa wizara wamesema kuwa mafunzo hayo yamewezesha kutambua namna ya kujipima na kuweka malengo yanayo weza kupimika.