Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wizara ya Katiba na Sheria

Ujenzi wa Jengo la Wizara Wafikia Asilimia 80

Imewekwa: 29 Dec, 2023
Ujenzi wa Jengo la Wizara Wafikia Asilimia 80

Na William Mabusi - WKS Dodoma

Ujenzi wa jengo la Wizara ya Katiba na Sheria linalojengwa Mji wa Serikali Mtumba limefikia asilimia themanini (80).

Taarifa hiyo imetolewa na Bw. Ibrahimu Chatila Mtaalam Mwelekezi kutoka Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) kwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria Dkt. Khatibu Kazungu tarehe 29 Desemba, 2023 alipotembelea maendeleo ya ujenzi huo. Aidha, Bw. Chatila amemtaka Mkandarasi wa ujenzi huo SUMA JKT kutobweteka kwa hiyo asilimia themanini kwani mradi huo ni miongoni mwa miradi ambayo Mkandarasi analipwa kwa wakati.

Akitoa maelekezo baada kukagua maendeleo ya ujenzi huo Dkt. Kazungu amesema “jitihada mlizoonesha hadi kufikia hatua hii ongezeni bidii na hasa baada ya kupokea vifaa vyenu vya ujenzi ambavyo bado viko bandarini.”

Kabla ya kufanya ukaguzi wa ujenzi Dkt. Kazungu akiwa na Menejimenti ya Wizara hiyo walikutana na kufanya mazungumzo na Wakandarasi kutoka SUMA JKT na Wataalam wa Majengo kutoka TBA.