Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wizara ya Katiba na Sheria

Wanafunzi Wafanya Mjadala Juu ya Msaada wa Kisheria

Imewekwa: 24 May, 2024
Wanafunzi Wafanya Mjadala Juu ya Msaada wa Kisheria

Na Lusajo Mwakabuku – WKS Njombe

Wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Mbeyela iliyopo Mkoani Njombe Mjini leo 24 Mei, 2024 wameonesha umahiri wao katika kudadavua masuala mbalimbali walipokuwa wakifanya mjadala juu ya msaada wa kisheria huku mada ikisema "Je jamii inafahamu juu ya Msaada wa Kisheria?" Mjadala huu umeandaliwa na Timu ya Msaada wa kisheria kutoka katika Kampeni ya Msaada wa Kisheria inayokusudiwa kuzinduliwa siku ya Jumapili tarehe 26 Mei, 2024 katika viwanja vya Stendi ya Zamani Njombe mjini.