Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wizara ya Katiba na Sheria

WANAWAKE  DODOMA WANUFAIKA NA HUDUMA ZA MSAADA WA KISHERIA

Imewekwa: 09 Mar, 2026
WANAWAKE  DODOMA WANUFAIKA NA HUDUMA ZA MSAADA WA KISHERIA

Mkuu wa  Mkoa wa Dodoma, Mhe. Rosemary  Senyamule, ameipongeza Wizara ya  Katiba na Sheria kwa juhudi  za kuwasaidia wanawake kupata haki zao kupitia kampeni ya Msaada wa Kisheria ya Mama Samia. 

Mhe. Senyamule ametoa pongezi hizo leo tarehe 8 Machi 2026 katika maadhimisho ya siku ya wanawake duniani ambapo katika mkoa wa  Dodoma kilele cha Maadhimisho hayo  kimefanyika katika Wilaya ya Kongwa.

Mhe. Senyamule  amesema  kuwa  jitihada zilizofanywa na wizara kwa nchi nzima zinaashiria dhamira ya Serikali ya kuimarisha upatikanaji wa haki kwa wananchi hususani Wanawake na inasaidia kuongeza uelewa wa masuala ya kisheria na kutoa fursa kwa  wanawake kushughulikia changamoto mbalimbali za kisheria zinazowakabili katika jamii. 

Katika maadhimisho hayo, wanawake kutoka Wizara ya Katiba na Sheria wameungana na wanawake wengine kuadhimisha siku hiyo kwa kutoa huduma ya msaada wa kisheria bila malipo  kwa wananchi