Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wizara ya Katiba na Sheria

Wanawake wa Wizara ya Katiba na Sheria Washiriki Maadhimisho ya Siku ya Wanawake

Imewekwa: 09 Mar, 2023
Wanawake wa Wizara ya Katiba na Sheria Washiriki Maadhimisho ya Siku ya Wanawake

Wafanyakazi wanawake wa Wizara ya Katiba na Sheria wameadhimisha siku ya Wanawake Duniani Kwa kuungana na wanawake wengine kutoka Wizara na Taasisi mbalimbali za Serikali na binafsi katika maadhimisho hayo kimkoa yaliyofanyika katika Wilaya ya Kondoa.

Maadhimisho hayo yamefanyika Machi 08, 2023 ambapo Mgeni Rasmi alikuwa Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dkt. Rosemary Senyamule.

Watumishi hao wameshiriki kwenye maandamano yaliyopokelewa na Mgeni Rasmi wakiwa na mabango yenye ujumbe mbalimbali.

Dkt. Senyamule wakati akiongea na watumishi wanawake kutoka ofisi mbalimbali amewaasa kujiamini na kuwa imara ili waweze kutimiza malengo yao bila kusubiri kusukumwa kwani uwezo wanao wa kufanya mambo makubwa kwa ajili ya jamii yao.

Maadhimisho ya siku ya Wanawake Duniani kwa mwaka 2023 yamebeba na kauli mbiu "ubunifu na mabadiliko ya teknolojia chachu katika kuleta usawa wa kijinsia.”