Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wizara ya Katiba na Sheria

Waziri Chana Ashiriki Mkutano wa Baraza la Vyama vya Siasa

Imewekwa: 03 Jan, 2024
Waziri Chana Ashiriki Mkutano wa Baraza la Vyama vya Siasa

Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chana leo tarehe 03 Januari 2024 ameshiriki Mkutano Maalum wa Baraza la Vyama vya Siasa unaoshirikisha Wadau wa Demokrasia ya Vyama Vingi kujadili Miswada ya Sheria za Uchaguzi na Sheria za Vyama vya Siasa iliyosomwa kwa mara ya kwanza Bungeni tarehe 10 Novemba, 2023.

Akifungua mkutano huo Mgeni Rasmi Makamu wa Kwanza wa Rais Zanzibar, Mhe. Othman Masoud Othman amewasihi Wadau na Washiriki wote kuitumia fursa hiyo vizuri kwa kutoa maoni yenye tija kwa ajili ya kujenga Taifa na kusema msingi mzuri wa kukubaliana ni mtu kuwa jasiri wa kusema wazo lake na kusikiliza mawazo ya wengine na kukubali wazo lililo bora zaidi kwa manufaa ya Taifa.