Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wizara ya Katiba na Sheria

Wizara 23 zaungana kutokomeza TB.

Imewekwa: 22 Mar, 2023
Wizara 23 zaungana kutokomeza TB.

Na Lusajo Mwakabuku WKS.

Katika kuhakikisha dhamira ya kupambana na hatimaye kuitokomeza TB na vichochezi vyake inakamilika, ushirikiano wa Sekta mbalimbali za Serikali zaidi ya zile zinazohusika na afya pamoja na vipaumbele thabiti vya kisiasa katika ngazi za juu za uongozi vina nafasi kubwa katika kuumaliza ugonjwa huu nchini.

Ni kwa mtazamo huo wa Serikali uliopelekea Wizara 23 kuingia makubaliano ya kuunda Mfumo wa Uwajibikaji wa Sekta mbalimbali (Multisectoral Accountability Framework - MAF) uliotiwa Saini na wawakilishi wa Wizara hizo, tarehe 21 Machi, 2023 Jijini Dodoma.