Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wizara ya Katiba na Sheria

Wizara imejipanga kuendelea kujenga Mahakama nchini - Pauline Gekul.

Imewekwa: 20 Jun, 2023
Wizara imejipanga kuendelea kujenga Mahakama nchini - Pauline Gekul.

Na. George Mwakyembe. WKS – Dodoma.

Naibu Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Pauline Gekul amesema Wizara imejipanga kundelea na ujenzi wa Mahakama nchini kwa mwaka wa fedha 2023/2024 na tayari Wizara imejipanga kujenga zaidi ya mahakama 60.

Mheshimiwa Gekul amesayema hayo alipokuwa akijibu swali la Mhe. Nashoni Bindyanguze Mbunge wa Kigoma Kusini. Mheshimiwa Gekul amesema kwa mwaka wa fedha 2024/2025 Wizara itajenga Mahakama ya Mwanzo katika eneo la Mgambo ambalo ndiyo Makao Makuu ya Tarafa ya Buhingu.

Naye Mbunge wa Arusha Mjini Mhe. Mrisho Gambo aliuliza swali la nyongeza kwa Mhe. Naibu Waziri Gekul kutaka Kujua ujenzi wa Mahakama ya Mwanzo katika Kata ya Terati. Mheshimiwa Gekul amemhakikishia kuwa katika mwaka wa fedha 2023/2024 ujenzi wa Mahakama ya Kata ya Terati ni Kata mojawapo zitajengwa.  

Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Manyara Mhe. Asia Halamga aliuliza swali kutaka kujua ujenzi wa Mahakama eneo la Minjingu Mkoani Manyara. Mhe. Naibu Waziri Gekul amemtoa wasiwasi na kwamba hilo eneo tayari liko kwenye mpango wa ujenzi wa Mahakama kwa mwaka fedha unaokuja.

Naye mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Shinyanga Mheshimiwa Christine Mzava ameomba Wizara kufanya ukarabati  wa Mahakama za Kata ya Usanda na Samuye kwani zimejengwa tokea enzi za mkoloni, Mheshimiwa Gekul  amemhakikishia  kuwa Mahakama hizo zitafanyiwa ukarabati .