Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wizara ya Katiba na Sheria

Wizara Itaendelea Kutoa Ushirikiano Utekelezaji wa MTAKUWWA II – Dkt. Chana

Imewekwa: 15 May, 2024
Wizara Itaendelea Kutoa Ushirikiano Utekelezaji wa MTAKUWWA II – Dkt. Chana

Na William Mabusi – WKS Dodoma

Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chana amesema Wizara yake itaendelea kushirikiana na Wizara za Kisekta, Taasisi za Serikali, Asasi za Kiraia, Wadau wa Maendeleo na wananchi katika kutekeleza Mpango Kazi wa Taifa wa Kutokomeza Ukatili dhidi ya Wanawake na Watoto Awamu ya Pili (MTAKUWWA II 2024/25 – 2028/29) kuhakikisa kwamba haki kwa wanawake na watoto inapatikana kwa wakati na kwa ufanisi kupitia huduma ya msaada wa kisheria.

Dkt. Chana ameyasema hayo alipokuwa akitoa salaam na tamko la Wizara kwenye Maadhimisho ya Siku ya Familia na Uzinduzi wa Mpango Kazi wa Taifa wa Kutokomeza Ukatili dhidi ya Wanawake na Watoto Awamu ya Pili, Mei 15, 2024 Jijini Dodoma.

“Wizara itaendelea kutoa huduma ya msada wa kisheria, kuweka mazingira wezeshi ya upatikanaji haki, kufanya mapitio ya sheria kubainisha maeneo yanayohitaji kufanyiwa marekebisho, kuweka sera na kanuni zinatoa ulinzi kwa wanawake na watoto ili kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake na watoto na makundi maalumu.” Amesema Dkt. Chana.

Aidha, Chana. Pindi amesema Wizara itaendelea kuratibu na kutekeleza mapendekezo ya Tume ya kuangalia jinsi ya kuimarisdha Taasisi za haki jina nchini, Kuwajengea uwezo watekelezaji wa sheria ili waweze kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake na watoto, Kuendelea kuratibu na kutekeleza Kampeni ya Kisheria ya Mama Samia katika mikoa yote nchini.