Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wizara ya Katiba na Sheria

WIZARA YA KATIBA NA SHERIA TANZANIA YASAINI MKATABA WA USHIRIKIANO NA WIZARA YA SHERIA JAPAN

Imewekwa: 22 Aug, 2025
WIZARA YA KATIBA NA SHERIA TANZANIA YASAINI MKATABA WA USHIRIKIANO NA WIZARA YA SHERIA JAPAN

Katibu Mkuu Wizara ya Katiba na Sheria Eliakim Chacha Maswi Agosti 21, 2025 ametia saini mkataba wa ushirikiano kati ya Wizara ya Katiba na Sheria ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Wizara ya Sheria ya Japan. 

Utiaji saini Mkataba wa Ushirikiano kati ya Wizara ya Sheria ya Japan na Wizara ya Katiba na Sheria ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania umeshuhudiwa na Makamu wa Waziri wa Sheria wa Japan Morimoto Hiroshi na Katibu Mkuu Eliakim Chacha Maswi 

Katika hafla ya utiaji saini na mkutano uliofuata, Viongozi wa wizara hizo walibadilishana mawazo juu ya kukuza ushirikiano katika ya sheria na haki