Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wizara ya Katiba na Sheria

Wizara Yawapiga Msasa Waratibu wa Msaada wa Kisheria Nchini

Imewekwa: 15 Jan, 2025
Wizara Yawapiga Msasa Waratibu wa Msaada wa Kisheria Nchini

Wizara ya Katiba na Sheria imeendelea kuchukua hatua madhubuti katika kuhakikisha huduma za msaada wa kisheria kupitia Kampeni ya Msaada wa Kisheria ya Mama Samia (MSLAC) zinafikia Watanzania kwa ufanisi. Katika hatua ya kuimarisha utekelezaji wa kampeni hiyo, mafunzo maalum yametolewa kwa waratibu wa MSLAC kutoka maeneo mbalimbali nchini. Tarehe 14 Januari, 2025.

Mafunzo hayo yanafanyika kwa muda wa siku mbili katika Chuo cha Uongozi Mwl. Nyerere Kibaha, Pwani, yamewalenga waratibu wa kampeni kwa lengo la kuwaongezea ujuzi na maarifa ya jinsi ya kusimamia, kuratibu, na kufikisha huduma za msaada wa kisheria kwa wananchi kwa ufanisi zaidi.