Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wizara ya Katiba na Sheria

MAADHIMISHO YA WIKI YA UTUMISHI WA UMMA 2025, WIZARA YA KATIBA NA SHERIA ITASHIRIKI.

12 Jun, 2025

Wizara ya Katiba na Sheria, itashiriki katika Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma, yatakayofanyika katika Viwanja vya Chinangali Park Jijini Dodoma, Kuanzia tarehe 16 Hadi 23 Juni, 2025.

Wizara inawakaribisha wananchi na wakaazi wa jiji la Dodoma na Mikoa jirani kutumia fursa hii kupata huduma mbalimbali ikiwa ni pamoja na huduma za Masuala ya Utumishi na Utawala, Msaada wa Kisheria Bure, Elimu ya Haki za Binadam pamoja na Elimu ya Uraia na Utawala Bora.

"Himiza matumizi ya mifumo ya kidijiti ili kuongeza upatikanaji wa taarifa na kuchagiza uwajibikaji"