Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wizara ya Katiba na Sheria

UZINDUZI WA KAMPENI YA MSAADA WA KISHERIA YA MAMA SAMIA DAR ES SALAAM TAREHE 16 JUNI 2025

09 Jun, 2025

*Zimebaki siku saba TU* 

 

Kuelekea Uzinduzi wa Kampeni ya Msaada wa Kisheria ya Mama Samia katika Mkoa wa Dar es Salaam katika viwanja vya Zakhem Mbagala tarehe 16 Juni, 2025 ambapo Mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa. 

Wananchi na wakazi wote wa jiji la Dar es Salaam mnakaribishwa kupata elimu na Msaada wa Kisheria Bure kabisa. 

Uonapo tangazo hili tafadhali mjulishe na mwenzako naye amwambie na mwenzie pia!

#Msaadawakisheriakwamaendeleoyajamii#