Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wizara ya Katiba na Sheria

SIKU YA KIMATAIFA YA HAKI ZA BINADAMU – 10 DISEMBA, 2025, Kaulimbiu: “HAKI NA WAJIBU KUELEKEA DIRA 2050”

10 Dec, 2025

Leo tarehe 10 Disemba, 2025 Tanzania inaungana na Dunia, kusherehekea Siku ya Kimataifa ya Haki za Binadamu, tukikumbuka kwamba haki na wajibu ni msingi wa maendeleo endelevu, mshikamano wa kijamii, na utawala bora.  Siku ya tarehe 10 Disemba, ilipitishwa na Azimio la Baraza la Umoja wa Mataifa kuwa Siku ya Haki za Binadamu kwa kuwa ni tarehe ambayo Tangazo la Kimataifa la Haki za Binadamu la mwaka 1948 (Universal Declaration of Human Rights) lilipitishwa na Baraza la Umoja wa Mataifa.