Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wizara ya Katiba na Sheria

Makondo Afanya Ziara ya Kikazi Iringa

Imewekwa: 04 Aug, 2023
Makondo Afanya Ziara ya Kikazi Iringa

Katibu Mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria Bi. Mary Makondo amefanya ziara ya kikazi mkoani Iringa ambapo katika ziara hiyo amefanikiwa kushiriki mafunzo ya mfumo wa NeST yaliyotolewa na Wataalam kutoka PPRA.

Aidha, Katibu Mkuu ametembelea timu ya Wataalam wa PPRA wanaojenga na kutoa huduma za mfumo wa NeST na akawapongeza huku akiwataka waongeze juhudi katika kuhakikisha mfumo unakuwa rafiki na hivyo kuboresha taratibu za manunuzi zitakazowezesha taifa kuboresha huduma za Serikali kwa wananchi kwa ujumla.

Katika hatua nyingine akiwa Mkoani Iringa, Bi. Makondo ametembelea na Kuzungumza na Wafanyakazi wa Ofisi ya Taifa ya Mashtaka Mkoani Iringa na kujadili mambo mbalimbali yahusuyo utendaji wao wa kazi, Muono mbele, Mafanikio na Changamoto zao.