Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wizara ya Katiba na Sheria

Makondo Azindua Mafunzo ya Mifumo ya TEHAMA

Imewekwa: 22 Aug, 2023
Makondo Azindua Mafunzo ya Mifumo ya TEHAMA

Katibu Mkuu Wizara ya Katiba na Sheria Bi. Mary Makondo amezindua mafunzo ya Mifumo ya TEHAMA yaliyoandaliwa na Shirika la Mtandao wa Watoa Huduma za Msaada wa Kisheria la (TANLAP) Jijini Dodoma tarehe 22 Agosti, 2023.

Akiongea katika hafla hiyo iliyofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Hoteli ya Morena, Katibu Mkuu amesisitiza matumizi ya TEHAMA katika kuwafikia wanyonge na kuwapa huduma za msaada wa Kisheria kote nchini huku akiwaasa washiriki wa mafunzo hayo kushiriki kikamilifu Kampeni ya Kitaifa ya Msaada wa Kisheria ya Mama Samia yaani Mama Samia Legal Aid Campaign inayofanyika kote nchini.