WAZIRI ULEGA APOKEA TAARIFA YA UTEKELEZAJI WA KAZI ZA WIZARA KWA ROBO YA KWANZA
Waziri wa Katiba na Sheria, Mhe. Abdallah Hamis Ulega (Mb), leo Novemba 24, 2026, amekutana na Menejimenti ya Wizara hiyo, inayoongozwa na Katibu Mkuu, Dkt. Seif Abdallah Shekalaghe, kwa ajili ya kupokea na kujadili taarifa ya utekelezaji wa shughuli za Wizara kwa kipindi cha robo ya kwanza ya mwaka wa fedha 2026/2027.
Kikao hicho kilichohudhuriwa pia Naibu Waziri wa Katiba na Sheria, Mhe. Zainab Athuman Katimba (Mb), kililenga kupitia hatua zilizofikiwa katika utekelezaji wa majukumu na programu mbalimbali za Wizara, pamoja na kutathmini maendeleo ya utekelezaji wa malengo yaliyowekwa.
Baada ya kupokea taarifa hiyo, Mhe. Ulega ameipongeza Menejimenti na wataalamu wa Wizara kwa kazi nzuri wanayoifanya katika kutekeleza majukumu yao, huku akiwataka kuongeza kasi na ufanisi katika utendaji ili kuhakikisha malengo ya Serikali yanafikiwa, hususan katika kuboresha utoaji wa huduma kwa wananchi.
Aidha, Waziri Ulega amemuelekeza Katibu Mkuu kuhakikisha programu ya “Sema na Waziri” inayotarajiwa kufanyika mapema mwezi Desemba,inaratibiwa vyema, ikiwemo kuhakikisha hoja na kero mbalimbali zilizowasilishwa na wananchi zinajibiwa na Wananchi wanapatiwa mrejesho wa hoja walizowasilisha, ili kuimarisha mawasiliano kati ya Wizara na wananchi pamoja na kuongeza uwajibikaji katika utoaji wa huduma.