Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wizara ya Katiba na Sheria

Ndumbaro Afanya Ziara ya Kikazi Malinyi

Imewekwa: 13 Aug, 2023
Ndumbaro Afanya Ziara ya Kikazi Malinyi

Waziri wa Katiba na Sheria Dkt. Damas Ndumbaro amefanya ziara ya kikazi katika Wilaya ya Malinyi iliyopo Mkoa wa Morogoro kwa lengo la kutembelea Wasaidizi wa Kisheria ambapo tarehe 12/08/2023 alitembelea ofisi ya Wasaidizi wa Kisheria Malinyi (Malinyi Paralegal Unity) na kukutana na Uongozi wa Kituo hicho ambacho kimekua na msaada mkubwa katika Wilaya hiyo yenye migogoro ya wakulima na wafugaji. 

Katika ziara hiyo, Mhe. Ndumbaro akiambatana na Mkuu wa Wilaya ya Malinyi bwana Sebastian Waryuba na Uongozi wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya ya Malinyi Mkoani Morogoro wamejadili namna ya kushughulikia masuala mbalimbali ya upatikaji haki Wilayani hapo.