Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wizara ya Katiba na Sheria

SEMA NA WAZIRI YAZIDI KUTIBU CHANGAMOTO ZA WANANCHI

Imewekwa: 15 Apr, 2026
SEMA NA WAZIRI YAZIDI KUTIBU CHANGAMOTO ZA WANANCHI

Waziri wa Katiba na Sheria, Mhe. Dkt. Juma Zuberi Homera, ameendelea na programu ya kuwahudumia wananchi wenye changamoto mbalimbali za kisheria kupitia Kituo cha Huduma kwa Mteja cha Wizara hiyo, leo Aprili 15, 2026 Mtumba Jijini Dodoma

Kupitia programu hiyo wananchi wamezungumza na kuwasilisha changamoto zao yakiwemo masuala ya ardhi,ndoa,ukatili wa kijnsia,mirathi  pamoja na madai.

Akizungumza wakati wa huduma hiyo, Mhe. Dkt. Homera ameeleza kuwa mpango huo ni utekelezaji wa maelekezo ya  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, yenye lengo la kuhakikisha haki inapatikana kwa kila mwananchi na kuwawezesha kufikia malengo yao kupitia mfumo wa haki ulio wazi na jumuishi.

Aidha Dkt. Homera amesisitiza kuwa programu hiyo itaendelea tena Aprili 22, 2026 ambapo pamoja na kupokea changamoto mpya, atatoa mrejesho wa changamoto zilizoripotiwa Aprili 15 kupitia program ya Sema na Waziri.