Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wizara ya Katiba na Sheria

WANANCHI KUHUDUMIWA KWA KASI YA 5G

Imewekwa: 25 Feb, 2026
WANANCHI KUHUDUMIWA KWA KASI YA 5G

Katibu Mkuu  Wizara ya Katiba na Sheria Ndg. Eliakim Maswi amewataka watumishi kuongeza kasi ya kutoa huduma kwa Wananchi kutokana  na kupatiwa vitendea kazi vya kisasa na vinavyoendana na mabadiliko ya kidigitali. 

Maswi aliyasema hayo tarehe 23 Februari, 2026 wakati akitoa vitendea kazi kwa watumishi wa wizara ya katiba na sheria katika hafla iliyofanyika katika ofisi za wizara Mtumba jijini Dodoma. 

Katika hatua nyingine Maswi  amewapongeza watumishi hao ambao ni Maafisa Kumbukumbu, Waandishi Waendesha Ofisi, Maafisa usafirishaji, Wasaidizi wa Kumbukumbu pamoja na Wasaidizi wa Ofisi kutambua umuhimu wa kazi yao na unyeti katika kuhakikisha Wizara inaendelea kufanya vizuri na kutoa huduma bora kwa Wananchi 

Kwa upande wake  Naibu Katibu Mkuu wa Wizara Dkt. Franklin Rwezimula amesisitiza umuhimu wa Watumishi hao kuchangamkia fursa mbalimbali za kujiendeleza kielimu kwani elimu haina mwisho.