WANANCHI MBALIMBALI WAJITOKEZA KUPATA HUDUMA ZA KISHERIA KATIKA MAONESHO YA SABASABA

Ikiwa ni siku ya nne tangu kuanza rasmi kwa Maonesho ya Kimataifa ya Kibiashara jijini Dar es Salaam, Wananchi mbalimbali wameendelea kujitokeza kupata Huduma za Kisheria katika banda la Wizara ya Katiba na Sheria jijini, Dar es Salaam.
Akizungumza katika mwendelezo wa shughuli za Utoaji wa Huduma katika Banda hilo, Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Haki za Binadamu Beatrice Mpembo amesema kuwa Wizara imejipanga kuendelea kutoa Elimu kwa Wananchi kupitia Idara zilizopo chini ya Wizara ili kuhakikisha kila Mwananchi anapata elimu .
"Wizara kazi yake kubwa ni kusimamia majukumu yote yanayohusu Katiba na Sheria.Katika Maonesho ya Sabasaba tunazo Idara mbalimbali ikiwemo Idara ya Katiba na Ufuatiliaji Haki,Idara ya Sheria kwa Umma, Idara ya Haki za Binadamu, Idara ya Msaada wa Kisheria na Kitengo cha Utajiri wa Asili na Maliasili za Nchi.Napenda kuwakaribisha Wananchi kufika na kujipatia elimu lakini pia kwa wenye uhitaji wa Msaada wa Kisheria na utatuzi wa migogoro tupo na Mama Samia Legal Aid katika Maonesho haya."amesem Beatrice.