Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wizara ya Katiba na Sheria

Bajeti Zizingatie Utekelezaji wa 4R za Mhe. Rais – Dkt. Chana

Imewekwa: 06 Feb, 2024
Bajeti Zizingatie Utekelezaji wa 4R za Mhe. Rais – Dkt. Chana

Na William Mabusi – WKS Dodoma

Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chana ameziagiza Taasisi za Wizara hiyo kuhakikisha zinazingatia pamoja na mambo mengine ya maendeleo lakini pia utekelezaji wa R4 za Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan.

Dkt. Chana ametoa agizo hilo wakati alipokutana na Wakuu wa Taasisi na Watendaji Wakuu wa Taasisi za Wizara, Wakurugenzi kutoka Wizarani na kupitishwa kwenye maoteo ya Bajeti ya mwaka fedha 2024/25 kwa Taasisi hizo tarehe 06 Februari, 2024 kwenye ofisi za Bunge Jijini Dodoma.

”Katika kipindi hiki cha kukamilisha maandalizi ya bajeti kwa mwaka wa fedha 2024/25 kila Taasisi na Mkuu wa Taasisi atwambie namna ambavyo amejipanga kuzitekeleza zile R4 za Mhe. Rais. Pangeni kufanya mageuzi na maboresho makubwa kwenye matumizi ya TEHAMA, Kufanya tathmini na mapitio ya sheria mbalimbali, Kuongeza visibility kwa maana ya kutangaza Taasisi zenu na Kuendelea kutoa elimu kwa umma, Kuwajengea uwezo watumishi.” Alisema Dkt. Chana huku akihimiza pia Taasisi hizo kuongeza mashirikiano na Wadau wa Maendeleo kwenye ufadhili wa miradi ya maendeleo.