• Maswali/
  • Mrejesho
  • English

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Wizara ya Katiba na Sheria

(MoCLA)

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Dira na Dhamira
    • Historia ya Wizara
    • Menejimenti
    • Majukumu Yetu
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Utawala
    • Muundo wa Wizara
    • Idara na Vitengo
      • Kitengo cha Uhasibu na Fedha
      • Kitengo cha Tehama
      • Idara ya Utawala na Rasilimali Watu
      • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
      • Idara ya Sera na Mipango
      • Idara ya Huduma ya Kisheria kwa Umma
      • Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
      • Idara ya Katiba na Ufuatiliaji Haki
      • Kitengo cha Ununuzi na Ugavi
      • Divisheni ya Haki za Binadamu
      • Natural Wealth and Resources Observatory Unit
  • Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Hotuba
    • Maktaba ya picha
    • Maktaba ya Video
    • Habari
    • Matukio
    • Matangazo
  • Machapisho
    • Katiba
    • Fomu Mbalimbali
    • Tafiti
    • Miongozo
    • Taarifa Mbalimbali
    • Sera
    • Sheria Mbalimbali
      • Katiba na Haki za Binadamu
      • Sheria za Jinai
      • Sheria za Madai
      • Sheria za Ardhi
      • Sheria za Mazingira
      • Sheria za Mirathi
      • Sheria za Utawala
      • Sheria za Biashara
      • Sheria za Rasilimali za Nchi na Madini
      • Sheria za Masaidiano na Mataifa Mengine
      • Sheria za Kimataifa
      • Sheria za Mabaraza na Usuluhishi
      • Sheria za Marekebisho ya Sheria Mbalimbali
  • Ununuzi
    • Taarifa ya Matarajio ya Ununuzi
    • Machapisho ya Tuzo za Zabuni
    • Mpango wa Mwaka wa Unununzi
    • Tangazo la Zabuni
  • Huduma Kupitia Mtandao
    • Mfumo wa Kuomba Kufungua Mashauri Nje ya Muda
    • Mfumo wa Kupokea Malalamiko
    • Usajili wa Watoa Huduma za Upatanishi, Majadiliano, Maridhiano na Usuluhishi
  • Huduma za Msaada wa Kisheria
    • Usajili wa Watoa Huduma za Msaada wa Kisheria
    • Mfumo wa Kuomba Msaada wa Kisheria
  • Sheria Blog

KAMPENI YA MSAADA WA KISHERIA KUFANYIKA NCHI NZIMA: DKT. KAZUNGU

Imewekwa: Wednesday 25, January 2023

KAMPENI YA MSAADA WA KISHERIA KUFANYIKA NCHI NZIMA: DKT. KAZUNGU

Serikali imejipanga kufanya kampeni ya Msaada wa Kisheria nchi nzima itayolenga kutoa elimu juu ya masuala mbalimbali yanayohusiana na sheria kwa watanzania wote.

Kauli hiyo imetolewa na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria Dkt. Khatibu Kazungu alipokuwa akifungua kikao kazi cha wajumbe wa Kamati ya maandilizi ya kampeni hiyo tarehe 24 Januari, 2023 Jijini Dodoma.

“Wananchi wengi bado hawana uelewa wa kutosha kuhusu masuala ya kisheria hali inayopelekea wengi wao kukosa haki zao, kutokuzipata kwa wakati au kuzipata kwa gharama kubwa sana.” Alisema Dkt. Kazungu.

Kampeni hiyo ambayo imepewa jina la _Mama Samia Legal Aid Campaign_ itatoa elimu ya kisheria kwa wataalam katika ngazi mbalimbali za kijamii na kwa wananchi wote ili kurahisisha taratibu zinazotakiwa kufuatwa wakati wa utoaji wa Haki na pia Haki iweze kutolewa kwa wakati.

Akitaja baadhi ya maeneo ya kuzingatia wakati wa utoaji elimu, Dkt. Kazungu alisema masuala ya ukarimu wa kijinsia, mirathi, masuala ya ardhi na haki za binadamu ni sehemu ya maeneo muhimu yanayogusa jamii na yanatakiwa kutafutiwa ufumbuzi kwa haraka sana.

Aidha, Dkt. Kazungu amehimiza ushirikiano miongoni mwa wadau wa Serikali na wasio wa Kiserikali na kuwataka kutumia weredi, uzoefu na ujuzi wao katika utekelezaji wa kampeni hii katika ngazi za kitaifa na kijamii ili katika kuhakikisha maeneo yote yanafikiwa na hivyo kuleta matokeo makubwa kwa haraka.

“Tunapopanga kutekeleza kampeni hii tuzingatie kwamba imebeba taswira ya Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Kwa kukubali kutumia jina lake Mhe. Rais ametuamini kuwa tutafanya kazi hiyo kwa uadilifu wa hali ya juu, tutafanya kazi iliyo njema na hivyo kulinda heshima yake kama Kiongozi Mkuu wa Taifa letu.” Aliongeza Dkt. Kazungu.

Aidha, amesema kampeni hiyo izingatie azma ya Mhe. Rais katika kulinda haki za kikatiba, utawala wa sheria, na haki za binadamu huku akiwaahidi kuwa Wizara ya Katiba na Sheria itatoa ushirikiano wa kutosha katika kufikia malengo yaliyowekwa katika kutekeleza kampeni hii.

Kamati hii inayoongozwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria kama Mwenyekiti na Bi. Lulu Ng’wanakilala Mkurugenzi Mtendaji wa LSF kama Makamu Mwenyekiti imekutana kwa lengo la kuendelea na maandalizi ya kampeni hiyo ikiwa ni pamoja na kubainisha mahitaji, kazi zitakazotekelezwa, na majukumu ya kila mdau.

Matangazo

  • KUTOA MAONI KUHUSU UBORESHAJI WA MFUMO WA SHERIA NCHINI NA ELIMU YA UANASHERIA KWA VITENDO

    ... Oct 19, 2022

  • MAOMBI YA KUSAJILIWA KWENYE MAHAKAMA YA AFRIKA YA HAKI ZA WATU KWA MAWAKILI WANAOTOA HUDUMA ZA KI... Jun 01, 2022

  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI TUME YA UTUMISHI WA MAHAKAMA

    Matangazo Zaidi

Habari Mpya

  • ​ARDHI YA TANZANIA NI YA UMMA NA SIO YA MTU BINAFSI- DKT. NDUMBARO

    ​ARDHI YA TANZANIA NI YA UMMA NA SIO YA MTU BINAFSI- DKT. NDUMBARO

    Jan 30, 2023
  • ​NDUMBARO AZINDUA KITABU CHA MASUALA YA AJIRA NA SHERIA ZA KAZI

    ​NDUMBARO AZINDUA KITABU CHA MASUALA YA AJIRA NA SHERIA ZA KAZI

    Jan 26, 2023
  • KAMPENI YA MSAADA WA KISHERIA KUFANYIKA NCHI NZIMA: DKT. KAZUNGU

    KAMPENI YA MSAADA WA KISHERIA KUFANYIKA NCHI NZIMA: DKT. KAZUNGU

    Jan 25, 2023
  • ​MAONESHO YA WIKI YA SHERIA: WATATUZI WA MIGOGORO KWA NJIA MBADALA WAANZA KUSAJILIWA KIELEKTRONIKI.

    ​MAONESHO YA WIKI YA SHERIA: WATATUZI WA MIGOGORO KWA NJIA MBADALA WAANZA KUSAJILIWA KIELEKTRONIKI.

    Jan 23, 2023
  • Soma Habari zaidi
Tanzania Census 2022
  • Video
  • Albamu
  • 5 Pics
  • 2 Pics

Wasiliana Nasi

Wizara ya Katiba na Sheria

Mji wa Serikali,Mtumba

S.L.P. 315,

DODOMA.

Masijala: barua@sheria.go.tz

Simu: +255 26 2310021

Nukushi: 255 26 2321679
Barua pepe: km@sheria.go.tz

  • Sera Ya Faragha
  • Angalizo
  • Ramani Ya Tovuti
  • Maswali
  • Barua Pepe

© 2023 Wizara ya Katiba na Sheria. Haki zote zimehifadhiwa..
Imesanifiwa, Imetengenezwa, na Mamlaka ya Serikali Mtandao (eGA) na Inaendeshwa na Wizara ya Katiba na Sheria