Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wizara ya Katiba na Sheria

Kasi ya Ujenzi Iendane na Ubora: Dkt. Chana

Imewekwa: 17 Nov, 2023
Kasi ya Ujenzi Iendane na Ubora: Dkt. Chana

Na William Mabusi – WKS Dodoma

Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chana amekagua maendeleo ya ujenzi wa jengo la ofisi za Wizara ambao umefikia asilimia 79 linaojengwa Mji wa Serikali Mtumba Dodoma, na kumtaka Mkandarasi kuongeza kasi huku akizingatia ubora.

Ukaguzi huo ameufanya tarehe 17 Novemba, 2023. “Kwenye ujenzi wa majengo haya tunashindana hivyo ukiona mwenzio ameweka vioo nawe unajiuliza la kwangu linawekwa vioo lini,” alisema Dkt. Chana huku akitahadharisha pamoja na mambo mengine upatikanaji wa maji kwenye jengo akitaka kuwepo na uwiano wa idadi ya watumishi na uwezo wa pampu ya kusukumuia maji ili yafike kwenye sakafu zote za jengo