Mgogoro wa Ardhi Uliodumu kwa Miaka Kumi Wapata Suluhu Karatu.

Mgogoro wa Ardhi uliodumu kwa takribani miaka kumi umepata utatuzi kupitia kampeni ya Mama Samia Legal Aid.
Akizungumza baada ya utatuzi wa mgogoro huo mratibu wa kampeni ya Mama Samia Legal Aid wilaya ya Karatu Dkt. Baraka Mkami Aprili 7, 2025 amesema kuwa wataalamu hao wamefanikiwa kutatua mgogoro huo na kukabidhi hati ya makubaliano ya kumaliza mgogoro wa Ardhi kati ya Bi. Veronica Damai na Pamphil Vicent.
Imeelezwa kuwa mgogoro huo kati ya Bi. Veronika na Bw. Vicent Pamhil ambapo mlalamikaji Bi. Veronika kwamba amepewa eno ambalo halina njia na amekuwa akipata changamoto ya kufika eno lake la nyumbani ndipo wanasheria hao walipo amua kumuita Pamphil nakukaa pamoja kwaajili ya mazungumzo na baada ya mazungumzo marefu ulipatikana muafaka ambapo bwana Pamphil alikubali kumuongezea Bi Veronica kipande cha mita tatu kwa upana na urefu mita 70 lakini pia kaka wa Bi Veronica anaejulika kwa jina La Damay aliamua kumpa bwana Pamphil kipande cha ardhi chenye upana wa mita moja na nusu na urefu wa mita 70 ili kufikia makubaliano ya mgogoro huo.