Mhe. Chana Atembelea Kituo Jumuishi cha Masuala ya Familia.
Mhe. Chana Atembelea Kituo Jumuishi cha Masuala ya Familia.
Imewekwa: 15 Nov, 2023
Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chana, tarehe 15 November 2023 ametembelea Kituo Jumuishi cha Masuala ya Familia Temeke kukagua shughuli mbalimbali za kiutendaji.
Akiwa Kituoni hapo Waziri Chana amepata fursa ya kutembelea maeneo mbalimbali ikiwemo Chumba maalumu ambacho kimetengwa kwa ajili ya akina mama kunyonyesha watoto wachanga wanapofika katika Kituo hicho kupata huduma.