Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wizara ya Katiba na Sheria

Mjane Arejeshewa Ardhi Aliyoporwa na Kijiji Miaka 10 Iliyopita.

Imewekwa: 03 Apr, 2025
Mjane Arejeshewa Ardhi Aliyoporwa na Kijiji Miaka 10 Iliyopita.

Jumapili tarehe 30 Machi, 2025 Timu ya Msaada wa Kisheria ya Mama Samia imeweza kumaliza mgogoro wa ardhi wa mjane Magdalena Kilase Samwenda ambao umedumu kwa zaidi ya miaka 10.

Wakati wa usikilizwaji wa shauri lake, Magdalena amelezea jinsi alivyosumbuka kwa zaidi ya miaka kumi akiitafuta haki yake mara baada ya uongozi wa kijiji cha Majengo kwa wakati huo kuchukua eneo lake ili kupata eneo la malisho la Kijiji cha Baraka.

Amesema kuwa Kampeni ya msaada wa kisheria sasa imewezesha kuipata haki yake na kumwezesha kumiliki kikamilifu eneo lake hilo wakati huu ambapo timu hiyo ya Mama Samia ikiendelea na kampeni ya Msaada wa Kisheria wa Mama Samia Legal Aid kata kwa Kata, leo ikiwa imewafikia wananchi wa kata 3 za Mto wa Mbu, Majengo na Migungani.