Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wizara ya Katiba na Sheria

Ndumbaro ajibu hoja za Mswada wa Marekebisho ya Sheria mbalimbali kwa Kamati

Imewekwa: 02 Jun, 2023
Ndumbaro ajibu hoja za Mswada wa Marekebisho ya Sheria mbalimbali kwa Kamati

Mheshimiwa Dkt. Damas Ndumbaro Waziri wa Katiba na Sheria ameshiriki katika Kikao cha Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria wakati Mwanasheria Mkuu wa Serikali Mhe. Jaji Dkt. Eliezer Mbuki Feleshi akiwasilisha majibu ya hoja mbalimbali zilizoibuliwa wakati akiwasilisha Mswada wa Sheria wa Marekebisho ya Sheria mbalimbali Jijini Dodoma, tarehe 01 Juni, 2023. Kikao hicho pia kimehudhuriwa na Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mhe. Nape Nnauye.