Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wizara ya Katiba na Sheria

RC SENYAMULE AIPONGEZA KATIBA NA SHERIA NA KUITAKA IJITANGAZE ZAIDI

Imewekwa: 05 Aug, 2025
RC SENYAMULE AIPONGEZA KATIBA NA SHERIA NA KUITAKA IJITANGAZE ZAIDI

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma ameipongeza Wizara ya Katiba na Sheria kwa namna wanavyo toa huduma mbalimbali za kisheria kwa wananchi huku akiwataka kuongeza uwanda wa kujitangaza ili wananchi waweze kufahamu huduma zinazotolewa.

Rc Senyamule ameyasema hayo mapema leo Agosti 5, 2025 wakati alipotembelea banda la Wizara hiyo katika maonesho na sikuu ya wakulima kitaofa yanayoendelea katika viwanja vya Nzuguni Jijini Dodoma.

“Nawapongeza kwa kazi nzuri mnayoifanya ya kuwahudumia wananchi kwa kutoa ushauri wa kisheria lakini mnatakiwa kuongeza uwanda ktaika kujitangaza ili wananchi wengi zaidi wafahamu kuwa mnatoa huduma za namna gani”, amesisitiza RC Senyamule.

Ameongeza kuwa wananchi wengi wamekuwa wakiwafuata viongozi mbalimbali ambao sio wataalamu wa kisheria kwa ajili ya ushauri wakati huku Huduma hizo zikitolewa na wizara bila gharama zozote.

“Kampeni ya Msaada wa Kisheria ya Mama Samia ina msaada sana kwa wananchi lakini bado haamjaitangaza vya kutosha, nawasihi ongezeni bidii wananchi wanatumbue kuwa msaada upon a ni bure kabisa ili wajae hapa kupata huduma hizi muhimu, wengi wanakimbilia kwetu kuomba ushauri wa kisheria kwakuwa hawajapata taarifa hizi”, amesisitiza RC Senyamule.

Kwa upande wake Mkurugenzi Msaidizi Ufuatiliaji na Uzingatiaji kutoka Idara ya  Msaada wa Kisheria Wizara ya Katiba na Sheria Osborn Paiss amesema kuwa wanaendelea kutekeleza kampeni ya Msaada wa Kisheria ya Mama Samia lakini pia wanatoa elimu kuhusiana na utajiri na maliasili za nchi ambazo ni mojawapo ya kazi zinazofanywa na Wizara ya Katiba na sheria.

“Lakini pia tunatembelewa na wananchi ambapo tunawapa ushauri mbalimbali ikiwemo mirathi, ardhi na mashauri ya ndoa, wengine wanapata elimu ya uraia na utawala bora,”amesema Paiss .

Pamoja na hayo amesema kuwa wanaendelea kujitangaza na kuwasihi wananchi waweze kufika katika eneo hilo ili waweze kupata msaada wa kisheria.

“Tunawakaribisha kwa wingi ili tuweze kuwasaidia kuwapa elimu kuhusu masuala mbalimbali ambayo yanawazunguka katika maeneo yao, na pia tuko na mawakili wote ambao wanaweza kuwasaidia katika utatuzi wa migogogro hivyo wananchi wajitokeze kwa wingi tutawahudumia vizuri sana” ameongeza Paiss

Aidha ameongeza kuwa huduma hizo zinatolewa bila malipo yoyote hivyo mwananchi mwenye changamoto yoyote yenye kuhitaji msaada wa kisheria asisite kufika katika banda la Wizara ya Katiba na Sheria  katika maonesho ya nanenane ili kupata msaada.