Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wizara ya Katiba na Sheria

TANZANIA NA RWANDA KUSHIRIKIANA  KATIKA SEKTA YA SHERIA

Imewekwa: 04 Sep, 2026
TANZANIA NA RWANDA KUSHIRIKIANA  KATIKA SEKTA YA SHERIA

Tanzania na Rwanda zimekubaliana kushirikiana  katika sekta ya sheria, ikihusisha utatuzi  wa migogoro kwa njia mbadala, uthibiti wa  uhalifu unaovuka mipaka pamoja kuimarisha huduma za msaada wa kisheria kwa wananchi.

Makubaliano hayo yamefikiwa katika mazungumzo kati ya Waziri wa Katiba na Sheria wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Juma Zuberi Homera, na Waziri wa Masuala ya Sheria na Mwanasheria Mkuu wa Jamhuri ya Rwanda, Mhe. Dkt. Emmanuel Ugirashebuja.

Nchi hizo zimekubaliana kubadilishana uzoefu na maarifa katika utatuzi wa migogoro, kukabiliana na uhalifu unaovuka mipaka na kuimarisha upatikanaji wa huduma za kisheria kwa wananchi, hususan wenye uhitaji.

Ushirikiano huu unaonesha dhamira ya Tanzania na Rwanda katika kuimarisha utawala wa sheria, mifumo ya haki na upatikanaji wa haki kwa wananchi wa nchi hizo mbili.

Mazungumzo hayo yamefanyika katika Ofisi za Wizara ya Sheria ya Rwanda jijini Kigali, yakihudhuriwa pia na Katibu Mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria, Dkt. Seif Shekalaghe, pamoja na Mkurugenzi wa Huduma za Kisheria kwa Umma, Ndg. Obadia Kameya.