Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wizara ya Katiba na Sheria

Tanzania Yashiriki Mkutano wa Upatikanaji Haki Nchini India

Imewekwa: 01 Dec, 2023
Tanzania Yashiriki Mkutano wa Upatikanaji Haki Nchini India

Na George Mwakyembe - WKS

Tanzania ni moja kati ya nchi washiriki katika mkutano wa kwanza wa kikanda kuhusu upatikanaji wa msaada wa kisheria, pamoja na Uimarishaji wa upatikanaji Haki katika nchi za ukanda wa kusini.

Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chana ameongoza washiriki kutoka Tanzania katika mkutano huo uliofanyika New Delhi nchini India kuanzia tarehe 27– 28 Novemba 2023 ukiwa unalenga kujadili masuala ya upatikanaji wa huduma za msaada wa kisheria katika kuimarisha upatikanaji haki nchini.

Katika Mkutano huo washiriki walipata nafasi ya kubadilishana uzoefu juu ya utekelezaji wa masuala ya huduma za msaada wa kisheria na jitihada mbalimbali zinazotumika katika kuhakikisha upatikanaji haki katika nchi zao pamoja na kuimarisha uhusiano na  baina  nchi washiriki na wadau mbalimbali wa haki katika ukanda wa kusini.