Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wizara ya Katiba na Sheria

Ukatili Wowote Wanaofanyiwa Watoto Utolewe Taarifa – Dkt. Chana

Imewekwa: 05 Apr, 2024
Ukatili Wowote Wanaofanyiwa Watoto Utolewe Taarifa – Dkt. Chana

Na Lusajo Mwakabuku - WKS Arusha

Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chana amewataka watanzania hususan Vyombo vya Habari kuongeza juhudi katika kuwalinda Watoto kwa kutoa taarifa za ukatili unaofanyika dhidi yao  ili hatua za kisheria ziweze kuchukuliwa.

Mhe. Chana ameyasema hayo leo tarehe 05 Aprili, 2024 wakati akihutubia Kikao cha Tatu cha Jukwaa la Haki Mtoto kilichofanyika katika ukumbi wa hoteli ya Four Points Jijini Arusha huku akiwataka washiriki kuongeza ushirikiano baina yao na Serikali katika kuhakikisha haki kwa watoto inapatikana.