Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wizara ya Katiba na Sheria

WAKUU WA IDARA NA VITENGO WAAGIZWA KUELEMISHA WATUMISHI KUHUSU SHERIA ZA UTUMISHI WA UMMA

Imewekwa: 02 Jul, 2025
WAKUU WA IDARA NA VITENGO WAAGIZWA KUELEMISHA WATUMISHI KUHUSU SHERIA ZA UTUMISHI WA UMMA

Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Katiba na Sheria, Dkt. Franklin Rwezimula amewaagiza wakuu wa Idara na Vitengo wa Wizara na Taasisi zilizo chini ya Wizara kuhakikisha wanatoa elimu na kuwaelimisha watumishi waliochini yao kuhusu uzingatiaji wa Sheria, Kanuni na Taratibu za Utumishi wa Umma ili kusaidia kuboresha utendaji kazi.

Dkt. Rwezaula ametoa maagizo hayo Julai 2, 2025 katika ukumbi wa Wizara jijini Dodoma alipokua akifungua mafunzo ya Mfumo wa Usimamizi wa Utendaji kazi katika Utmishi wa Umma (e-Utendaji) yanayotolewa na Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora.

Amesema wakuu wa Idara na Vitengo wanahakikisha wanazingatia suala la uwajibikaji, Sheria, Kanuni na Taratibu za Utumishi wa Umma katika utekelezaji wa majukumu yao ili kuongeza ufanisi wa utendaji kazi na utekelezaji wa majukum yao ya kila siku.

Dkt Rwezimula ameongeza kuwa kupitia mafunzo haya wakuu wa Idara na Vitengo watapata fursa ya kujifunza na kujadili kuhusu hatua ya kufanya tathmini ya utendaji kazi wa watumishi kwa mwaka (Employee Performance Assessment) ili kuboresha utendaji kazi na uwajibikaji katika Idara na vitengo wanavyovisimamia.

Aidha Dkt. Rwezaula ameipongeza Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora kwa kuona umuhimu wa kutoa mafunzo haya yatakayowasaidia wakuu wa Idara na Vitengo kufanya utekelezaji wa mfumo wa e-utendaji hususan katika eneo la tathmini ili kuwasaidia watumishi kutambua wajibu wao na kufikia malengo yaliyokusudiwa. 

“Ninatoa shukrani zangu za dhati kwa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora kwa kuona umuhimu wa kutoa Mafunzo haya yatakayowasaidia kutekeleza mfumo wa e-utendaji” amesema Dkt. Rwezaula.
 
Ameongeza kuwa “Natoa rai kwenu kuzingatia mafunzo haya muhimu ili kila mmoja wenu aweze kufanya utekelezaji wa mfumo wa e-utendaji kwa ukamilimifu hasusan katika eneo la tathimini ili kila mtumishi aliyeko chini yenu aweze kutambua wajibu katika kufikia malengo yaliyokusudiwa” amesisitiza.