Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wizara ya Katiba na Sheria

Wanafunzi wa Nanja Sekondari Wanufaika na Kampeni ya Msaada wa Kisheria

Imewekwa: 09 Apr, 2025
Wanafunzi wa Nanja Sekondari Wanufaika na Kampeni ya Msaada wa Kisheria

Wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Nanja, wilayani Monduli, wamenufaika na kampeni ya msaada wa kisheria kupitia mpango wa Mama Samia Legal Aid, unaolenga kuwaelimisha wananchi, hususan wanafunzi, kuhusu haki zao za kisheria.

Kampeni hii, iliyoendeshwa na wanasheria wa kujitolea kwa ushirikiano na serikali, imewapa wanafunzi uelewa juu ya masuala muhimu kama haki za watoto, sheria za elimu, unyanyasaji wa kijinsia, na taratibu za kisheria wanazopaswa kufuata iwapo watakumbana na changamoto zinazohitaji msaada wa kisheria.

Nao wanafunzi walioshiriki, wameeleza kampeni hiyo imemfungua macho kuhusu namna ya kutafuta msaada wa kisheria pindi anapokutana na changamoto.

Mpango wa Mama Samia Legal Aid unaendelea kutekelezwa katika maeneo mbalimbali nchini, ukiwa na lengo la kuwafikia wanafunzi wengi zaidi ili kuwawezesha kuwa na uelewa wa kisheria unaowawezesha kujilinda na kudai haki zao kwa mujibu wa sheria.