Waziri Dkt. Pindi Chana Afanya Mazungumzo na Balozi wa Switzerland
Waziri Dkt. Pindi Chana Afanya Mazungumzo na Balozi wa Switzerland
Imewekwa: 22 Jul, 2024

Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Balozi. Dkt. Pindi Chana leo Julai 22, 2024 amekutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Switzerland nchini Tanzania aliyemaliza muda wake Bw. Didier Chasot.
Kikao hicho kilichofanyika Jijini Dar es Salaam, kililenga kujadili namna ya kuendeleza mashirikiano katika kulinda haki za binadamu hususan katika masuala ya uimarishaji wa utajiri asili na maliasilia za nchi, kuendeleza na kulinda haki za binadamu na mapitio ya mfumo wa haki za binadamu.