Wizara ya Katiba na Sheria Inatekeleza Vyema Maono ya Rais Samia- Amon Mpanju

Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Bw. Amon Mpanju ameipongeza Wizara ya Katiba na Sheria kwa kuyaweka kikamilifu maono ya Rais Samia Suluhu Hassan kwenye vitendo, hasa kwa namna ambavyo Wizara hiyo imekuwa sehemu ya kupambana na ukatili kwa jamii.
Wakili Mpanju ametoa rai hiyo Machi 28, 2025 wakati wa uzinduzi wa kampeni ya Msaada wa kisheria ya Mama Samia Jijini Arusha, akitoa rai kwa wananchi hasa wajane, walemavu na wagane kujitokeza kwa wingi kwenye Kampeni hiyo itakayokwenda kwenye Wilaya zote za Mkoa wa Arusha mara baada ya uzinduzi wake.
Mpanju pia kwa niaba ya Wizara ya Maendeleo ya Jamii, jinsia, wanawake na makundi maalum, ametoa pongezi kwa Waziri wa Katiba na sheria Dkt. Damas Ndumbaro kwa namna ambavyo wizara yake inatekeleza mpango wa taifa wa kutokomeza ukatili ambapo sekta ya sheria kupitia Msaada wa kisheria kwa wananchi ilitakiwa kuwafikia wananchi, kuwasikiliza na kutatua malalamiko yao.