Wizara Yapokea Magari Tisa Kati ya Kumi Kurahisisha Huduma za Kisheria kwa Wananchi
Wizara Yapokea Magari Tisa Kati ya Kumi Kurahisisha Huduma za Kisheria kwa Wananchi
Imewekwa: 31 Dec, 2024
Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Dkt. Damasi Ndumbaro amewataka watumishi wa wizara ya Katiba na Sheria kufanya kazi kwa weledi na ufanisi kutokana na Serikali kuweka mazingira wezeshi kwa ajili ya kurahisisha utendaji wao wa kazi.
Waziri Ndumbaro ameyasema hayo wakati akipokea magari tisa kwa ajili ya watumishi wa wizara hiyo katika kutekeleza Kampeni maalum ya Msaada wa kisheria ya Mama Samia Legal Aid campaign.
Amesema magari hayo yatasaidia kurahisisha utendaji kazi kwa Mikoa sita kwa wakati mmoja hivyo watendaji kuendelea kuwa waadilifu.
Magari tisa kati ya kumi yamezinduliwa tarehe 20 Desemba, 2024 ambapo lengo ni katika kurahisisha shughuli za utendaji kwa watumishi wa wizara hiyo.