Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wizara ya Katiba na Sheria

IMPACT

Mradi Improving Accountability through fighting Corruption and Increased Access to Justice – (IMPACT)

Mradi huu ni kuwezesha Sheria ya Msaada wa Kisheria inatekelezwa ipasavyo ili kuongeza wigo na kuimarisha mazingira ya wananchi kuifikia haki hususan kwa makundi maalum ikiwemo wanawake, pamoja na kuimarisha mapambano dhidi ya rushwa. Matokeo ya awali ya mradi huu ni kuwa na watoa huduma ya Msaada wa Kisheria wenye uwezo na tija ya utoaji wa huduma ya Msaada wa akisheria kwa umma na kuwa mifumo rasimi ya utoaji wa huduma ya msaada wa kisheria nchini. Matokeo ya kati ya mradi huu ni wananchi wenye mahitaji ya huduma ya msaada wa sheria nchini wanapata huduma hiyo sehemu sahihi na kwa wakati. Matokeo ya muda mrefu wa mradi huu haki inapatikana kwa maendeleo endelevu ya taifa.