Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wizara ya Katiba na Sheria

TAARIFA KWA UMMA: USAJILI WA WATOA HUDUMA ZA MSAADA WA KISHERIA TANZANIA BARA(LAPs)

01 Sep, 2026 Pakua

TAARIFA KWA UMMA

Usajili wa Watoa Huduma za Msaada wa Kisheria Tanzania Bara (LAPs)

Msajili wa Watoa Huduma za Msaada wa Kisheria anapenda kutoa taarifa kwa Mashirika yote ya Msaada wa Kisheria (LAPs) yanayofanya kazi Tanzania Bara kuhusu maboresho ya mfumo wa usajili.

Ili kuhakikisha matakwa ya kisheria yamezingatiwa na kuboresha utoaji wa huduma kwa jamii, Watoa Huduma wote wanatangaziwa  kwamba, Wizara imekamilisha ujenzi wa  mfumo mpya wa kidijitali wa NaLIS. Hivyo, Watoa Huduma wanataarifiwa kuanza kukamilisha usajili au kuhuisha taarifa zao na taarifa za Wasaidizi wao wa Kisheria (Paralegals) kwa kutumia mfumo huo. Taarifa kamili na maelekezo ya  utekelezaji  ni kama  ifuatavyo;

  1. Watoa Huduma za Msaada wa Kisheria ambao bado hawajasajiliwa wanatakiwa kujisajili kwenye mfumo wa NaLIS (https://nalis.sheria.go.tz);
  2. Watoa Huduma wote ambao awali walisajiliwa katika mfumo wa zamani wanaelekezwa kuingia kwenye mfumo mpya wa NaLIS (https://nalis.sheria.go.tz)  ili kuhuisha taarifa zote za mashirika yao.  Wakati wa kuhuisha taarifa zote shirika linapaswa pia kuhuisha taarifa zote za Wasaidizi wa Kisheria (Paralegals). Zoezi hili lifanyike kuanzia tarehe ya taarifa hii hadi kufikia tarehe 30 Septemba, 2026.
  3. Endapo shirika lako lipo kwenye orodha ya mashirika ambayo hayajakamilisha taarifa za awali hapa chini, tafadhali wasiliana nasi kupitia: Barua pepe: support.nalis@sheria.go.tz, na kwa namba ya simu: 0712096434.

 

Imetolewa na:

 

MSAJILI WA MSAADA WA KISHERIA

WIZARA YA KATIBA NA SHERIA

31 AGOSTI, 2026