Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wizara ya Katiba na Sheria

Balozi Dkt. Pindi Chana Akutana na Balozi wa Urusi Nchini

Imewekwa: 27 Sep, 2023
Balozi Dkt. Pindi Chana Akutana na Balozi wa Urusi Nchini

Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chana amekutana na Balozi wa Urusi nchini Mhe. Andrey Avetisyan na kufanya majadiliano ya namna bora ya kuendelea kushirikiana na Tanzania katika maeneo mbalimbali hasa katika Sekta ya Sheria.

Kikao hicho kimefanyikia tarehe 27/09/2023 katika Ukumbi wa Ofisi za Wakala wa Usajili, Udhamini na Ufilisi (RITA) Jijini Dar es Salaam ambapo moja ya eneo lililogusiwa katika mazungumzo hayo ni kuimarisha mifumo ya Haki ambapo Balozi Avetisyan ameahidi kuendelea kutoa ushirikiano katika maeneo ya kisheria nchini na kusaidia katika uboreshaji wa sheria.

Katika majadiliano hayo Kwa upande wa Tanzania, Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chana amesema Tanzania inaendelea kutekeleza Mipango mbalimbali chini ya Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ikiwemo Kampeni maarufu ya Mama Samia Legal Aid inayolenga kuwasaidia Watanzania kufikiwa na haki, usajili wa matukio muhimu ya binadamu ikiwemo vizazi, ndoa na vifo lengo likiwa ni kuhakikisha huduma inafika kwa Wananchi huku Wizara yake ikisimamia Utawala wa Kisheria na masuala ya usuluhishi.